MSHAMBULIAJI wa zamani wa timu ya Simba na kipenzi cha mashabiki wengi wa wekundu hao, Emmanuel Okwi, amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia klabu ya Simba.
Habari za ndani zilizopatiklana jana, Mshambuliaji huyo ataanza kuonekana katika mazoezi ya timu hiyo kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Huu utakuwa ni msimu wa tatu tofauti wa Okwi kuichezea Simba ambapo mara ya mwisho Simba ilimuuza mshambuliaji huyo kwa dau kubwa katika klabu ya Etoile du Sahel ya nchini Tunisia.
Okwi alianza kuichezea Simba mwaka 2009 hadi 2012 na kuondoka kutimkia kwenye klabu ya Etoile Du Sahel ya nchini Tunisia, akarejea tena msimu wa 2013/2014 na kusaini mkataba wa miaka miwili na klabu ya Yanga na alidumu kwa kipindi cha nusu msimu kabla ya kurejea tena Simba.
Msimu wa 2014/2015, Okwi akiwa Simba alicheza nusu msimu kabla ya klabu hiyo kumuuza kwenye klabu ya Sonderjsky ya nchini Denmark ambako hakupata mafanikio na timu hiyo na sasa ameamua kurejea tena kwa wekundu hao.
Akizungumzia juu ya kurejea kwa mshambuliaji huyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Klabu ya Simba, Zacharia Hanspope, alisema usajili wa Okwi umekamilika kwa asilimia 80 lakini tayari gaazeti hili lina taarifa kuwa mshambuliaji huyo ameshasaini mwaka mmoja kuitumikia timu hiyo.
Alisema Simba ina uwezo wa kumleta mshambuliaji yoyote na kwamba sio kwamba wanashindwa kumleta straika mwingine tofauti na Okwi, wanalazimika kumrejesha kwakuwa ni mzoefu wa ligi ya Tanzania tayari alishawahi kuchezea katika klabu za Simba na Yanga.

EmoticonEmoticon