Millionaire  Ads

Thursday, November 17, 2016

MOURINHO KUMNASA DEMBELE

Tags


Mourinho Kumnasa Dembele


MANCHESTER, England


MANCHESTER United inamnyatia kinda wa Celtic ya Scotland, Mousa Dembele ili kuimarisha kikosi chake kwenye kipindi cha msimu wa kiangazi.


Manchester United imefikia hatua hiyo baada ya kinda huyo kuonesha kiwango kikubwa kwenye mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia chini umri wa miaka 21, kinda huyo alifunga bao kwa mpira wa adhabu.

Manchester United imetuma wawakilishi kwenye mazoezi ya Celtic ili kuhakikisha wanapata saini ya kinda huyo kabla ya mwisho wa mwezi huu.


Mashetani hao wekundu wamemtuma Skauti David Friilo kwa ajili ya kuangalia uwezo wa kinda huyo mwenye asili ya Afrika.


Chanzo cha habari kutoka England kimesema kuwa Dembele anatarajia kuanza mazungumzo na Manchester United hivi karibuni kwa ajili ya uhamisho wa dirisha dogo la usajili mwezi Januari mwakani.

Mourinho amemfananisha kinda huyo na Straika wake wa zamani Didier Drogba kutokana na aina yake ya uchezaji akiwa uwanjani.

Mchezaji huyo ana thamani ya pauni milioni tano kutokana na kiwango chake kuongezeka siku hadi siku.

Mashetani hao wekundu wa jiji la Machester wanahitaji saini ya kinda huyo ili kuziba nafasi ya Mholanzi Memphis Depay anayetarajia kuondoka kwa mkopo kwenye klabu ya Everton.


EmoticonEmoticon