Millionaire  Ads

Sunday, November 13, 2016

Mjue Alex Iwobi

Tags

ALEX  IWOBI
 
Kinda la Arsenal linalofananishwa na  Nwanko Kanu.
 
Ni binamu wa Nguli wa Zamani wa Nigeria, Jay Jay Okocha.
 
NA ABDUL DUNIA
 
SOKA ni mchezo namba moja kwa kupendwa duniani.
 
Mchezo huo umejizolea sifa kutokana na aina ya uchezaji wake huku ukiwa umefanya watu wengi kuwa maarufu na kuheshimika.
 
Miongonoi mwa watu ambao wamekuwa maarufu kwa ajili ya soka ni mfalme wa soka duniani Pele, fundi Zinedine Zidane, Ronaldinho, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.
 
Watu hao wamekuwa maarufu sana kutokana na usakataji wao mzuri wa mchezo huo wakiwa uwanjani.
 
Kuna watu ambao walitokea kwenye bara la Afrika na walifanikiwa kufuta tabia za wazungu ambao walikuwa ni wabaguzi wa rangi  kutokana na usakataji wao bora wa soka.
 
Roger Milla, Nwanko Kanu, Samuel Etoo, George Weah na Didier Drogba wameweza kuzibadilisha hisia za wazungu kwenye ubaguzi wa rangi kutokana na uchezaji wao wa mchezo huo.
 
Wachezaji hao waliweza kuheshimika sana na mashabiki wa ulaya na wengine walitengenezewa hadi masanamu kwenye timu zao kutokana na kuhesimika kwao.
 
Uzuri wa mchezo wa soka hauangalii  mwili wala ukubwa wa umri wa mtu hivyo ni mchezo unaotumia akili nyingi kuliko nguvu.
 
Kwa kipindi hiki kuna makinda yanayowika ligi kuu England (EPL) wenye asili ya Afrika.

Alex Iwobi ni mmoja wa makinda kutoka Afrika ambaye amekuwa mwiba kwenye Ligi hiyo.
Kinda wa Arsenal Alex Iwobi alizaliwa may 3, 1996 kwenye mji wa Lagos nchini Nigeria.
Ni mchezaji wa pili kwenye familia yake baada ya binamu yake nguli wa zamani wa Nigeria na klabu ya Fulham ya England Jay Jay Okocha.
Iwobi anacheza nafasi ya winga na mshambuliaji wa kati ambaye amekuwa akiiwakilisha vizuri Nigeria nchini England kwa kipaji chake anachokionesha.
Maisha yake
Iwobi alizaliwa Lagos kabla ya kwenda England akiwa na umri wa miaka minne.
Ambapo alianza soka akiwa kwenye kituo maalum cha soka jijini humo nchini Nigeria.
Safari yake kwenye Soka
Iwobi alijiunga na Arsenal wakati akiwa anasoma shule ya msingi jijini London.
Alijumuishwa kwenye kikosi cha kwanza kama mchezaji asiyetumika wakati akiwa na umri wa miaka kumi na saba kwenye kombe la Ligi dhidi ya West Bromwich Albion Oktoba 25, 2013.
Alisaini mkataba wa muda mrefu akiwa na Arsenal Oktoba 2015 kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo inayonolewa na Kocha Profesa Arsenal Wenger.
Msimu wa 2015-2016
Oktoba 23, mwaka 2015, Iwobi aliingia kwenye kikosi cha kwanza cha Arsenal Wenger kwenye mchezo wa kombe la Ligi mzunguko wa 16 bora dhidi ya Sheffield Wednesday Siku nne baadae alicheza kwa mara ya kwanza Ligi kuu England kwenye ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Swansea City kwenye uwanja wa Liberty chini Wales akichukua nafasi ya Mesut Ozil kwenye dakika ya 85.
Tunaweza kusema kuwa Iwobi kama alikuwa na bahati na Arsenal baada ya kuingia kwenye mchezo wa Ligi ya mabingwa dhidi ya Bayern Munich waliochapwa 5-1.
Baada ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza kwenye mchzo dhidi ya Barcelona, kinda huyo alionesha kiwango cha hali ya juu kilichowaduwaza wachambuzi wengi wa soka barani ulaya.
Kinda huyo alianza kucheka na nyavu kwenye mchezo dhidi ya Everton na Watford.
Mashabiki walimbeza
Mashabiki wa Arsenal nchini England walijaribu kumlalamikia kocha wa kikosi hicho Arsenal Wenger kutokana na kumuamini kwake kinda huyo na kujaribu kumuingiza kwenye michezo migumu ikiwemo ule dhidi ya Bayern Munich na Barcelona ambayo yote Arsenal walipoteza.
Aanza Kukubalika
Kutokana na kipaji ambacho Iwsobi alikuwa anakionesha kwenye kila mchezo mashabiki wa Arsenal walianza kuvutiwa na huduma ya kinda ahuyo.
Kinda huyo aliendelea kuwika na Arsenal kwenye msimu uliopita ambapo alikuwa chachu kubwa ya ushindi wa kikosi hicho chenye maskani yake jijini London.
Afananishwa na Mkongwe Kanu
Binamu huyo wa Jay Jay Okocha amewahi kufananishwa na mkongwe wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria na klabu ya Arsenal, Nwanko Kanu kutokana na aina ya uchezaji wanaocheza.
Mashabiki wa Arsenal walimlazimisha Kocha walijaribu kumshawishi Arsenal Wenger kum,patia nafasi ya kudumu kwenye kikosi hicho kinda huyo kwa kuwa anaonesha kiwango kikubwa kuliko mshambuliaji wa timu hiyo, Olivier Giroud.
Atakata dhidi ya Chelsea
Kwenye mchezo uliopigwa hivi karibuni dhidi ya Chelsea, Arsenal ilishinda 3-0, Iwobi alionesha kiwango cha hali ya juu kilichowafanya mashabiki wengi kumshangilia huku wachambuzi wakimsifia kwa ubora wake aliokuwa nao kwenye soka.
Baada ya mchezo huo kumalizika chama cha soka England (FA), kilmzawadia kinda huyo tuzo ya mcheazji bora chipukizi wa mechi.
Timu ya Taifa
Baada ya kucheza timu ya taifa ya vijana kwenye timu ya England, Iwobi alichagua kucheza kwenye timu ya taifa ya Nigeria ambapo alipozaliwa.
Mchezo wake wa kwanza kwenye ti mu ya taifa ya Nigeria ulikuwa dhidi ya DR Congo Ocktoba 8, 2015 alichukua nafasi ya Ahmed Mussa kwenye dakika ya 57. 
Alichaguliwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Nigeria kilichoshiriki michuano ya Olimpiki jijini Rio de Janeiro, Brazil mwaka huu.
England wamgombania
Kabla ya kuamua kuchezea Nigeria, Iwobi alilazimishwa na kocha wa zamani wa England, Roy Hodgson kuwa akubali kujiunga na timu yake ya taifa lakini jitihada za kumshawishi zxiligonga mwamba baada ya kinda huyo kukubali kucheza Nigeria.


EmoticonEmoticon