Milambo yang'ara Mwanza
NA ABDUL DUNIA
BENDI ya Milambo ya Mwanza imeibuka mshindi wa mashindano ya kumsaka mkali wa muziki wa kizazi kipya (Bongo fleva) kwenye mkoa wa Mwanza.
Bendi hiyo inayohusisha wanamuziki wanne imeibuka kidedea baada ya kutangazwa mshindi wa mashindano hayo, jana mkoani humo.
Wanamuziki wanaounda bendi hiyo ni Rafael Yusto, William Simon 'Mr Champion', Almasi Salum na Vicent Zakaria Vice.
Akizungumza kwa njia ya simu jana, Meneja wa bendi hiyo, Hidaya Milambo alisema kuwa bendi yake ilistahili kupata ushindi huo bnaada ya kujifua kwa muda mrefu.
Alisema kuwa bendi yake ilifanya mazoezi kwa juhudi na ndio maana ikaibuka mshindi wa mashindano ya mkali wa bongo fleva mkoani Mwanza.
Aidha, Meneja huyo alisema kuwa vijana wake wamepania kufanya vizuri kwenye muziki wa Bongo fleva ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.
Hidaya Milambo amewataka mashabiki wa muziki wa bongo fleva kuiunga mkono bendi hiyo.
"Tunashukuru kwa kuwa tumepata ushindi wa mashindano ya mkali wa Bongo Fleva, tulistahili kushinda kwa kuwa tulijiandaa vema kuwakabili wapinzani wetu," alisema Meneja wa bendi hiyo.
Baada ya bendi hiyo kuibuka mshindi wa mashindano hayo walipata zawadi ya shilingi mil. 2 na laki tano kutoka kwa baadhi ya wadau wa muziki mkoani Mwanza.
Pia wadau mbali mbali wa muziki wa bongo fleva Mkoani humo waliahidi kuwasaidia vijana hao ili kufikia ndoto zao.
EmoticonEmoticon