Millionaire  Ads

Wednesday, November 16, 2016

karate yanoga

Tags

Karate yanoga


NA ABDUL DUNIA


CHAMA cha Karate Tanzania (TASHOKA),
kinatarajia kuandaa mashindano ya kuwasaka mabingwa wa mchezo huo ambao wataiwakilisha nchi kwenye michuano ya kimataifa.

Mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu na yatahusisha washiriki kutoka kila pande ya Tanzania.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa TASHOKA, Sensei Rwezaula, alisema kuwa watahakikisha wanaendesha mashindano hayo kwa misingi na katiba ya mchezo huo nchini.

Alisema watachagua mshindi aliyekuwa sahihi ili kupata bingwa atakayeiwakilisha nchini vizuri.

Aidha, Mwenyekiti huyo alisema kuwa watahakikisha wanatembea Tanzania nzima kwa ajili ya kutafuta vijana ambao wanaupenda mchezo wa Karate ili kuibua vipaji hivyo.

Rwezaula amewataka vijana kuupenda mchezo hio ili kuiwakilisha nchi kwenye mapambano ya kimataifa.

"Tunatarajia kuandaa mashindano ya Karate mwishoni mwa mwaka huu ili kupata wapambanaji watakaoweza kushiriki vema mapambano ya Taifa na Kimataifa kwa lengo la kuendeleza mchezo huo," alisema Rwezaula.

TASHOKA imepewa mamlaka na Baraza la Michezo la Taifa (BMT), linakikisha inaendesha mchezo huo kwa misingi ya katiba ya nchi ili kuibua vijana wenye vipaji vya mchezo wa Karate.


EmoticonEmoticon