Mghana Azam Anogewa
NA ABDUL DUNIA
STRAIKA mpya wa Azam FC , Samuel Afful amesema kuwa anafurahia kucheza soka nchi Tanzania kutokana na changamoto ya namba aliyokutana nayo.
Straika huyo Mghana ambaye alikuja kwa ajili ya majaribio kwenye Klabu ya Azam FC kwa sasa ameonekana kukubalika na mashabiki na viongozi wa Azam FC kutokana na soka bora alilolionyesha Juzi.
Mghana huyo alionyesha soka la aina yake kwenye Uwanja wa Azam Complex juzi kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Ruvu Shooting, Azam ilishinda 3-1 huku Afful akitupia moja.
Akizungumza Dar es Salaam, Samuel Afful, alisema kuwa ingawa ni mara yake ya kwanza kucheza Tanzania lakini amekumbana na changamoto ya ushindani kwenye kikosi hicho za Kocha Zeben Hernandez.
Afful alisema kuwa soka la Tanzania lina ushindani kuliko Ghana ambapo kwa kuwa kila timu inahitaji ushindi inapokutana.
"Mpira wa Tanzania una ushindani kuliko kwetu (Ghana) kwa kuwa kila timu ianahitaji ushindi lakini kwetu timu za usgindi zinajulikana mara kwa mara, mpira wa Tanzania uko juu," alisema Afful.
Straika huyo ametua wiki iliyopita akitokea Hasaacas ya Ghana ambapo alikuja na mchezaji mwenzake Agyei Attah kutoka Medeama aliyesajiliwa na Azam FC tangu msimu uliopita.
EmoticonEmoticon