Millionaire  Ads

Thursday, November 17, 2016

Hamilton kutwaa Ubingwa?

Tags

Nguli ampa tano Hamilton


LONDON, England


NGULI wa zamani wa Mbio za Magari yaendayo kasi Duniani, Langalanga, Ron Dennis amempa nafasi ya kutwaa ubingwa wa 'Formula One' dereva wa Merceds Benz, Lewis Hamilton kutokana na juhudi alizozionyesha kwenye michuano hiyo.


Hamilton alitwaa ubingwa wa Brazilian Grand Prix hivi karibuni baada ya kutoka kwenye majeraha ya goti.

Ron Dennis alisema kuwa anampa nafasi ya kutwaa ubingwa wa Dunia wa Formula One kutokana na juhudi anazoendelea kuzionyesha kwenye mbio mbali mbali za michuano hiyo.
 
Hadi sasa Hamilton ameshashinda kwenye mbio 52 tangu aanze mchezo wa Langa langa lakini anafutiwa na upinzani wa hali ya juu mbele ya dereva mwenzake wa Mercedes, Nico Rosberg.

Rosberg anaiongoza mbio hizo za Ubingwa wa Dunia akiwa na pointi 365 wakati Hamilton akiwa na alama 347 wakati wa tatu akiwa ni Daniel Riccuiardo ambaye ana pointi 342.


Hamilton atakuwa bingwa iwapo tu atashinda michuano ya mwisho huku Rosberg asiposhika kwenye nafasi tatu bora.


EmoticonEmoticon