ERIC DIER:
L Mtoto wa mcheza Tenisi anayemweka benchi Wayne Rooney, England
Aliwahi kutesa na Sporting CP ya Ureno, sasa yuko Spurs
LONDON, England
LIGI Kuu ya England (EPL) ni Ligi yenye msisimko, ushindani na changamoto ya hali ya juu.
Hiyo yote ni kutokana na timu mbalimbali zilivyoweza kujiandaa wakati wa maandalizi yake ya usajili kwa ujumla ili kujiweka fiti kwa michuano hiyo.
Miaka mitano iliyopita Ligi hiyo ilikuwa ngumu, tamu na aina yake kwa kuwa ilisheheni wachezaji mbalimbali wenye nguvu na uwezo wa kusakata kabumbu.
Kuna waliopita akina Benjamin Mwaluwali, Benny Mcarthy, Emmanuel Adebayor, Paul Schoels na wengine ambao walikuwa wakiongeza radha ya Ligi.
Walikuwepo watukutu akina Roy Keane, Patric Viera, Joey Barton na Michael Barack lakini sasa hawapo.
Kuondoka kwa mafundi na watukutu England kumechangia kwa kiasi kikubwa kuporomoka thamani halisi ya EPL.
Lakini sasa kuna wachezaji ambao wanakipiga EPL kwenye vilabu tofauti tofauti unaweza kujaribu kuwafananisha na mafundi wale walioondoka England.
Ndio, unaweza kuhisi kuwa utamu wa EPL miaka mitano iliyopita unarejea tena kutokana na baadhi ya wachezaji kufanya kweli kama wakongwe waliopita.
Wapo akina Mesut Ozili, Paul Pogba, Diego Costa, Sadio Mane na wengineo.
Lakini Uhuru Jumatatu, limekuandalia makala haya ili kukueleza maisha ya Kiraka Eric Dier anavyoifanya EPL kurejea kwenye utamu wake.
Ndio Dier ni mchezaji mwenye kiwango bora kwa sasa England ambaye amekuwa akiwakumbusha mashabiki wa Ligi hiyo duniani enzi za akina Xabi Alonso na Claudio Makelele.
Huyu ndiye Dier
Anaitwa Eric Jeremy Edger Dier, alizaliwa January 15 1994 kwenye jiji London nchini England.
Ni mwanasoka raia wa England anayekipiga Ligi Kuu England kwenye klabu ya Tottenham Hotspur pamoja na timu ya taifa ya England.
Alizaliwa kwenye kitongoji kidogo cha Cheltenham jijini Gloucedstershire nchini England.
Dier alihamia nchini Portugal na familia yake kipindi akiwa na umri wa miaka saba kutokana na Mama yake kupata kazi ya kuhudumia wachezaji uwanjani kwenye michuano ya Ulaya (UEFA EURO) iliyofanyika Ureno.
Dier aliishi mwaka mmoja katika jiji la Algarve kabla ya kuhamia jijini Lisbon kwa ajili ya makazi rasmi na familia yake.
Mwaka 2010, wazazi wake walirejea England wakati Dier aliendelea kuishi Ureno huku akiwa anaitumikia timu ya vijana ya Sporting CP ya nchini humo.
Dier ni Mjukuu wa Ted Croker ambaye ni katibu mkuu wa zamani wa Shirikisho la Soka England (FA) rais wa mji mdogo wa Cheltenham.
Vile vile Binamu yake ni Peter Croker ambaye ni mwanasoka wa zamani wa Charlton Athletic.
Amkana baba yake, ajiingiza kwenye soka
Unaweza kusema kuwa Dier alimkana baba yake kwa kuwa baba yake, Jeremy Dier ni mchezaji mkongwe wa zamani wa mchezo wa Tenisi nchini England.
Fundi huyo aliamua kujiingiza kwenye soka wakati akiwa na umri wa miaka saba nchini England wakati baba yake alitaka amrithishe kwenye mchezo wa Tenisi.
Maisha yake ya Soka
Wakati akiwa nchini Portugal Dier, alifanikiwa kuitumikia timu ya soka ya shule aliyokuwa anasoma ambapo alionesha kiwango cha hali ya juu hadi akajumuishwa kwenye timu ya vijana ya Sporting CP nchini humo wakati akiwa na miaka nane.
Dier alisaini mkataba wa miaka mitano kwenye klabu ya Sporting mwaka 2010 ili kuitumikia kwenye michuano mbali mbali ya ulaya.
Wakati Dier alipokuwa akiichezea Sporting, timu hiyo iliweza kuzifunga timu kongwe za England ambazo ni Arsenal, Tottenham Hotspur na timu aliyokuwa akiishabikia Dier wakati akiwa mtoto mdogo, Manchester United.
Mnamo January 2011, Dier alikubali kujiunga na Everton kwa mkopo.
Alipokuwa Everton kwa mkopo Dier alikuwa akicheza kikosi cha chini ya miaka 18 kutokana na umri wake kutomruhusu mkucheza timu ya wakubwa.
Dier na wenzake waliweza kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England chini ya miaka 18 kwenye msimu wa 2010- 2011.
Novemba 4 2012, Dier alifunga bao lake la kwanza akiwa na kikosi chake cha Sporting kwa mkwaju wa adhabu ndogo dhidi ya Benfica B.
Aitwa kikosi cha wakubwa
Novemba 11 2012, Dier alicheza mchezo wake wa kwanza na kikosi cha timu ya wakubwa Sporting CP akichukua nafasi ya Ricky van Wolfswinkel kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Ureno dhidi ya Braga.
Siku kumi na tano baadae, Dier alifunga bao lake la kwanza kwenye mchezo wa Ligi dhidi ya Moreirense ugenini wakati timu yake ikitoka sare ya mabao 2-2.
Atimkia Spurs
Agosti 2 mwaka 2014, Dier alisaini mkataba wa miaka mitano katika klabu ya Tottenham Hotspur kwa ada ya Pauni milioni 4.
Mashabiki wa Spurs haweakuamini kuwa Dier anaweza kutakata na kumnyima namba kiungo mkongwe wa zamani wa klabu hiyo Mualgeria Nabil Bentalleb kutokana na kiwango chake.
Mchezo wake wa kwanza kucheza akiwa na Spurs ulikuwa dhidi ya West Ham United kwenye msim u wa mwaka 2014-2015 ambapo alifunga bao pekee katika dakika za nyongeza.
Dier alianza kwenye kikosi cha kwanza March 1 mwaka 2015 ambapo Spurs ilifungwa 2-1 dhidi ya Chelsea kwenye mchezo wa fainali ya kombe la Ligi kwenye dimba la Wembley.
Dier alisaini mkataba mpya Septemba 9 mwaka jana wa kuitums hadi 2020.
Dier alianza kuaminiwa na kocha wa kikosi hicho Mauricio Pochettino ambapo alikmuwa akimuanzisha nafasi ya kiungo mkabaji.
Septemba 13 mwaka huu, Dier alisaini mkataa mpya utakaoweza kumbakisha Spurs hadi mwaka 2021.
Timu ya taifa ya England
Dier alianza kuitumikia timu yake ya taifa ya England chini ya umri wa miaka 19 mwaka 2012.
Shirikisho la Soka nchini Ureno kuitumikia Ureno lakini ilishindikana kutokana na mchezaji huyo kuwa mzalendo na nchi yake.
Dier alifunga bao lake la kwanza kwenye kikosi cha timu ya taifa ya chini ya umri wa miaka 18 baada ya Kocha wa kikosi hicho cha 'Three Lions' kumuanzisha kwenye mchezo dhidi ya Slovakia.
Baada ya kiwango chake kuimarika zaidi ya awali kocha wa kikosi cha England chini ya 21, Peter Tylor alimjumuisha kwenye kikosi chake kilichoshirikmi Kombe la Dunia mwaka 2013.
Kutokana na kucheza nafasi zaidi ya moja uwanjani Kocha wa kipindi hiko wa England alimtumia kama beki wa kulia kwenye kikosi hicho.
Novemba mwaka jana, Dier alichaguliwa kwenye kikosi cha wakubwa cha England na Kocha wa zamani Roy Hodgson kwa ajili ha mchezo wa kirafiki dhidi ya Hispania na Ufaransa.
Dier alianza kwenye mchezo dhidi ya Ufaransa uliochezwa kwenye uwanja wa Wembley ambapo alicheza kwa kiwango cha hali ya juu huku akiibuka mchezaji bora wa mchezo huo.
Alifunga bao lake la kwanza kwenyew timu ya taifa ya England mnamo March 2016, kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Ujerumani.
Dier aliitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya England kilichokwenda Ufaransa kucheza michuano ya Ulaya (UEFA EURO).
Alifunga bao kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Urusi kwa mkwaju wa adhabu ndogo uliokwenda moja kwa moja nyavuni.
Amuweka Rooney Benchi
Kipindi hiki Dier ndiye anayemweka benchi nahodha wa Kikosi hichi cha 'Three Lions', Wayne Marc Rooney kutokana na kuwa kipenzi cha mashab iki wa England.
Dier ni kipenzi cha mashabiki wa England kwa kuwa kiwango chake kina imarika siku hadi siku.
Afananishwa na Scholes, Keane
Aliweza kufananishwa na mkongwe wa zamani wa England na Manchester United Paul Scholes kutokana na aina ya uchezaji anavyocheza uwanjani.
Mashabiki wa England wanamfananisha Dier na kiungo mtukutu wa zamani wa Manchester United, Roy Keane kutokana na kulisakata soka vizuri
Nafasi anazocheza
Eric Dier ni kiraka kwa kuwa ana uwezo wa kucheza zaidi ya namba moja uwanjani.
Ana uwezo wa kucheza nafasi ya Kiungo mkabaji, beki wa kati na beki wa pembeni.