Millionaire  Ads

Thursday, March 2, 2017

SERENGETI BOYS KUNOLEWA NA NYOTA WA ZAMANI WA LIVERPOOL

Tags

JOHN BARNES.

MCHEZAJI mkongwe wa Liverpool ya England, John Barnes, amewasili nchini jana kwa ajili ya kushiriki katika shughuli mbalimbali za michezo ikiwamo kuwafunda wachezaji wa timu ya Taifa ya Vijana ya umri chini miaka 17 (Serengeti Boys).

Barnes amekuja nchini kwa mwaliko wa Benki ya Standard Chartered ambayo kesho itasheherekea miaka 100 tangu ilipoanzishwa mwaka 1917.

Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Sanjay Rughani, alisema anaamini ujio wa nyota huyo utasaidia kuhamasisha wachezaji chipukizi kufikia malengo yao kwa kuwa wachezaji wa kimataifa.

Rughani alisema amefurahi kuona timu kutoka sehemu mbalimbali zilichuana kuwania Kombe la Standard Chartered ambalo mabingwa wake wataenda kutembelea makao makuu ya Liverpool na kushuhudia wakicheza mechi mojawapo ya Ligi Kuu England.

Alisema mbali na kumualika mkongwe huyo, benki yao inajipanga kusaidia maandalizi ya Serengeti Boys ambayo baadaye mwaka huu itashiriki fainali za Afrika za Vijana zitakazofanyika Gabon.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Selestine Mwesigwa, alisema kuwa wanaamini mazungumzo atakayofanya mchezaji huyo yatawasaidia kiufundi wachezaji wa Serengeti Boys ambao wanatarajia kuchuana na wenzao wenye uzoefu wa kucheza michuano mbalimbali ya kimataifa.

Friday, February 17, 2017

MCHEZAJI WA ZAMANI WA YANGA SC NA TIMU YA TAIFA AFARIKI DUNIA

Tags
Mchezaji wa zamani wa Yanga na Taifa Stars afariki dunia ni baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Kiungo wa zamani wa klabu ya Yanga na timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ amefariki dunia alhamisi hii huko nyumbani kwao Mbeya.

Mchezaji huyo alikuwa amelazwa kwa muda mrefu hospitali ya Rungwe-Tukuyu Mbeya alikokuwa akipatiwa matibabu.

Wakati akicheza soka, Bonny aliwahi kuvitumikia vilabu vya Tanzania Prisons na Yanga kwa vipindi tofauti pamoja na timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.

Thursday, February 16, 2017

TIMU YA NGAYA KUTOKA COMORO YAWASILI KWA MECHI YA MARUDIANO NA YANGA SC

Tags
 Wachezaji wa Timu ya Ngaya ya nchini Comoro wakiwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam leo mchana kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya Yanga utakaofanyika kesho kutwa Uwanja wa Taifa. Katika mchezo wa awali uliofanyika Comoro Yanga ilishinda bao 5-1.

Picha ya pamoja na viongozi wao mara baada ya kuwasili uwanja  wa ndege wa Mwl. Julius Nyerere DSM.

SIMBA SC YASONGA HATUA YA NANE BORA KOMBE LA FA

Tags

Simba wamesonga hatua ya nane bora kombe la shirikisho maarufu kama Azam Federation baada ya kuifunga African Lyoni bao moja kwa bila.
Goli hilo lililoisogeza simba hatua ya nane bora limefungwa na Laudit Mavugo akipewa asist na Ibrahim Ajib dakika 57 kipindi cha pili.

Sunday, February 12, 2017

YANGA SC YAANZA KWA USHINDI WA KISHINDO COMORO

Tags

YANGA SC wameanza vizuri mawindo yao ya ubingwa wa Afrika, baada ya kwachapa wenyeji Ngaya Club de Mde mabao 5-1 jioni ya leo mjini Moroni, Comoro.

Ushindi huo unamaanisha Yanga watakuwa na shughuli nyepesi tu katika mchezo wa marudiano wiki ijayo mjini Dar es Salaam, kwani hata wakifungwa 3-0 watasonga mbele.

Kiungo Mzambia, Justin Zulu alifungua akaunti yake ya mabao Jangwani baada ya kusajiliwa msimu huu kwa kuifungia Yanga bao la kwanza dakika ya 43.

Kikosi cha Yanga kilichoanza leo Moroni na kuwachapa wenyeji 5-1

Winga machachari, Simon Happygod Msuva akaifungia Yanga bao la pili dakika ya 45 na Yanga ikaenda kupumzika inaongoza kwa mabao 2-0.

Mzambia mwingine, Obrey Chirwa akaifungia Yanga bao la tatu dakika ya 59, kabla ya Mrundi, Amissi Joselyn Tambwe kufunga la nne dakika ya 65 na Mzimbabwe Thabani Kamusoko kufunga la tabo dakika ya 73.

Ngaya walijipatia bao lao la kufutia machozi dakika ya 66 kupitia kwa Said Anfane Bourah Mohammed aliyetokea benchi kipindi cha pili.

Kikosi cha Ngaya kilikuwa; Said Mmadi, Said Hachim, Said Tothir, Adhepeau Denis Hubert, Ali Ahmada, Youssouf Ibrahim Moidjie, Zamir Mohammed, Mounir Moussa, Franck Said Abderemane, Rakoarimanana Falinurina na Chadhuili Mradabi.


Yanga SC; Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Hajji, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Justin Zullu, Simoni Msuva/Emmanuel Martin, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe/Juma Mahadhi, Obrey Chirwa na Haruna Niyonzima/Said Juma ‘Maka

Saturday, February 11, 2017

SAFU YA USHAMBULIAJI YA SIMBA SC NI MOTO WA KUOTEA MBALI

Tags

Muunganiko wa safu ya ushambuliaji ya simba sc wazidi kuimalika, baada ya matokeo ya mechi ya jana iliyochezwa uwanja wa taifa Dar es salaam kuibuka na ushindi wa magoli matatu bila kuruhusu nyavu zao kutikiswa na wapinzani wao Tanzania Prisons ya jijini Mbeya.
Muunganiko wa Laudit Mavugo na Ibrahim Ajibu wazidi kuimarika mara baada ya kupeana pasi za mwisho katika ufungaji wa magoli, ambapo Mavugo alitoa asist ya goli la pili kwa Ibrahim Ajibu kipindi cha kwanza dakika ya 28. Kipindi cha pili Ajibu naye alipiga krosi iliyozaa goli la tatu kwa simba likifungwa kwa kichwa na Mavugo na kuhitimisha idadi ya magoli matatu kwa bila.

MATOKEO YA MECHI ZILIZOCHEZWA JANA HISPANIA

Tags

 Real Betis 0:0 Valencia
 Alaves 0:6 Barcelona
Athletic Bilbao 2:1 Deportivo La
Coruna
 Osasuna 1:3 Real Madrid

MATOKEO EPL

Tags



 Arsenal 2:0 Hull City
ManchesterUnited 2:0 Watford
 Middlesbrough 0:0 Everton
Stoke City 1:0 Crystal Palace
Sunderland 0:4 Southampton
West Ham
United 2:2 West Bromwich
AlbionLiverpool 2:0 Tottenham
Hotspur

SIMBA YATUMA SALAMU JANGWANI

Tags
Simba sports club yarejea kileleni kwa tofauti ya pointi mbili ikiwa imetangulia mechi moja baada ya kuifunga timu ya Tanzania prisons ya Mbeya goli tatu kwa bila kupitia kwa Juma Luizio,Ibrahim Ajib na Laudit Mavugo.
Kwa idadi hiyo ya magoli kwa Wajela jela hao wa Mbeya ni salamu tosha kwa wapinzani wao watoto wa Jangwani 'wa kimataifa' watakapokutana tarehe 25.02.2017.Ambapo Yanga wapo Comoro kwaajili ya mechi ya kimataifa club bingwa Afrika dhidi ya timu ya Ngaya fc ya nchini humo.
Tags

Wafungaji ligi kuu Tanzania

Tags

Friday, February 10, 2017

SAMATA AREJEA UWANJANI NA KUIPA TIMU YAKE ZAWADI YA GOLI

Tags
Mchezaji wa kimataifa Mbwana Samata anayeichezea timu ya KRC GENK ya Ubelgiji amerejea vema uwanjani baada ya kuifungia timu yake bao la pili kwa kichwa, na kuifanya timu hiyo kuibuka na ushindi wa magoli matatu kwa bila dhidi ya St. Truiden. Akimalizia krosi iliyopigwa na Alejandro Pozuelo,pia goli la kwanza likifungwa Aljandro Pozuelo akipewa assist na Siebe Schrijvers na bao la mwisho likifungwa mnamo dakika ya 45 na Ruslan Malinovsky.

Timu ya Prisons ya Mbeya city yatishia kumfunga mnyama

Tags
Timu ya Prisons "Wajelajela" ya jijini Mbeya imesema iko tayari kwa ajili ya mechi dhidi ya Simba, itakayopigwa kesho JUmamosi katika dimba la Taifa dar es Salaam

 Wachezaji wa Prisons wakishangilia ushindi walioupata dhidi ya Simba katika mchezo wa mzunguko wa kwanza, ambapo Prisons ilishinda 2-1

Kocha Mkuu wa timu hiyo, Abdallah Mohammed amesema wamejiandaa vilivyo kuhakikisha wanafanya vizuri na kuendeleza ubabe kwa Simba kwa kunyakua pointi tatu katika mchezo huo.

"Tunajua Simba ni timu ngumu sana lakini tumejiandaa vizuri na tunataka ushindi hata kama kuna ugumu, tutapambana kuhakikisha tunafanya vizuri," amesema Mohammed.

Katika mzunguko wa kwanza, Simba walilala kwa mabao 2-1 mjini Mbeya na Prisons ikawa timu ya pili kuifunga Simba msimu huu baada ya African Lyon.

Ratiba ya mechi zitakazocheza wikendi hii

Tags

Ligi kuu ya Uiengereza itaendelea hapo kesho ikiwa ni wiki ya 25 tangu michuano hiyo ianze kutimua vumbi na ratiba kamili ni hii hapa chini huku mechi kali ikiwa ni kati ya Liverpool na Tottenham.

Jumamosi, Februari 11
1530 Arsenal v Hull City
1800 Manchester United v Watford
1800 Middlesbrough v Everton
1800 Stoke City v Crystal Palace
1800 Sunderland v Southampton
1800 West Ham United v West Bromwich Albion
2030 Liverpool v Tottenham Hotspu

Jumapili, Februari 12
1600 Burnley v Chelsea
1900 Swansea City v Leicester City

Jumatatu, Februari 13
2300 Bournemouth v Manchester City

Thursday, February 9, 2017

STARS KUSHUKA RANK ZA FIFA

Tags

TANZANIA imezidi kuporomoka katika orodha ya viwango vya soka inayotolewa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), kufuatia kuangukia nafasi ya 158 baada ya Januari.

Na hiyo inatokana na timu ya taifa, Taifa Stars kutokuwa na mchezo wowote wa kirafiki wa kimataifa tangu Desemba, licha ya kutofuzu Fainali za Kombe la Mataifa (AFCON) nchini.

Tanzania kuangukia nafasi ya 158 ikiwa na pointi 152 katika orodha ya Februari, 2017 inamaanisha imeshuka kwa nafasi mbili zaidi kutoka ya 156.

Pamoja na kuporomoka kwa nafasi mbili hadi ya 73, lakini Uganda wameendelea kuongoza kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati.

Na Uganda imeporomoka Januari kutokana na kutoshinda mechi katika Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka huu Gabon. Kenya ni ya pili kwa ukanda wa CECAFA ikiwa nafasi ya 87.

Mabingwa wapya wa Afrika, Cameroon wamepanda kwa nafasi 29 hadi ya 33, huku washindi wa pili Misri wamerudi juu hadi nafasi ya 23 baada ya kuporomoka miaka miwili iliyopita.

Argentina imeendelea kuongoza kwa ubora wa soka duniani, wakifuatiwa na mahasimu wao, Brazil nafasi ya pili na Ujerumani wa tatu.

Tanzania inaingia katika zama mpya sasa chini ya kocha Salum Mayanga, anayekuwa kaimu kocha Mkuu wa Taifa Stars akirithi mikoba ya Charles Boniface Mkwasa aliyeondolewa mapema mwezi huu.

Wednesday, February 1, 2017

Matokeo ya ligi kuu uingereza mechi zilizochezwa hapo jana,.

Tags
West Ham
United 0:4 Manchester
City
21:00 FT Manchester
United 0:0 Hull City
21:00 FT Stoke City 1:1 Everton