Millionaire  Ads

Thursday, March 2, 2017

SERENGETI BOYS KUNOLEWA NA NYOTA WA ZAMANI WA LIVERPOOL


JOHN BARNES.

MCHEZAJI mkongwe wa Liverpool ya England, John Barnes, amewasili nchini jana kwa ajili ya kushiriki katika shughuli mbalimbali za michezo ikiwamo kuwafunda wachezaji wa timu ya Taifa ya Vijana ya umri chini miaka 17 (Serengeti Boys).

Barnes amekuja nchini kwa mwaliko wa Benki ya Standard Chartered ambayo kesho itasheherekea miaka 100 tangu ilipoanzishwa mwaka 1917.

Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Sanjay Rughani, alisema anaamini ujio wa nyota huyo utasaidia kuhamasisha wachezaji chipukizi kufikia malengo yao kwa kuwa wachezaji wa kimataifa.

Rughani alisema amefurahi kuona timu kutoka sehemu mbalimbali zilichuana kuwania Kombe la Standard Chartered ambalo mabingwa wake wataenda kutembelea makao makuu ya Liverpool na kushuhudia wakicheza mechi mojawapo ya Ligi Kuu England.

Alisema mbali na kumualika mkongwe huyo, benki yao inajipanga kusaidia maandalizi ya Serengeti Boys ambayo baadaye mwaka huu itashiriki fainali za Afrika za Vijana zitakazofanyika Gabon.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Selestine Mwesigwa, alisema kuwa wanaamini mazungumzo atakayofanya mchezaji huyo yatawasaidia kiufundi wachezaji wa Serengeti Boys ambao wanatarajia kuchuana na wenzao wenye uzoefu wa kucheza michuano mbalimbali ya kimataifa.

Friday, February 17, 2017

MCHEZAJI WA ZAMANI WA YANGA SC NA TIMU YA TAIFA AFARIKI DUNIA

Mchezaji wa zamani wa Yanga na Taifa Stars afariki dunia ni baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Kiungo wa zamani wa klabu ya Yanga na timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ amefariki dunia alhamisi hii huko nyumbani kwao Mbeya.

Mchezaji huyo alikuwa amelazwa kwa muda mrefu hospitali ya Rungwe-Tukuyu Mbeya alikokuwa akipatiwa matibabu.

Wakati akicheza soka, Bonny aliwahi kuvitumikia vilabu vya Tanzania Prisons na Yanga kwa vipindi tofauti pamoja na timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.

Thursday, February 16, 2017

TIMU YA NGAYA KUTOKA COMORO YAWASILI KWA MECHI YA MARUDIANO NA YANGA SC

 Wachezaji wa Timu ya Ngaya ya nchini Comoro wakiwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam leo mchana kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya Yanga utakaofanyika kesho kutwa Uwanja wa Taifa. Katika mchezo wa awali uliofanyika Comoro Yanga ilishinda bao 5-1.

Picha ya pamoja na viongozi wao mara baada ya kuwasili uwanja  wa ndege wa Mwl. Julius Nyerere DSM.

SIMBA SC YASONGA HATUA YA NANE BORA KOMBE LA FA


Simba wamesonga hatua ya nane bora kombe la shirikisho maarufu kama Azam Federation baada ya kuifunga African Lyoni bao moja kwa bila.
Goli hilo lililoisogeza simba hatua ya nane bora limefungwa na Laudit Mavugo akipewa asist na Ibrahim Ajib dakika 57 kipindi cha pili.

Sunday, February 12, 2017

YANGA SC YAANZA KWA USHINDI WA KISHINDO COMORO


YANGA SC wameanza vizuri mawindo yao ya ubingwa wa Afrika, baada ya kwachapa wenyeji Ngaya Club de Mde mabao 5-1 jioni ya leo mjini Moroni, Comoro.

Ushindi huo unamaanisha Yanga watakuwa na shughuli nyepesi tu katika mchezo wa marudiano wiki ijayo mjini Dar es Salaam, kwani hata wakifungwa 3-0 watasonga mbele.

Kiungo Mzambia, Justin Zulu alifungua akaunti yake ya mabao Jangwani baada ya kusajiliwa msimu huu kwa kuifungia Yanga bao la kwanza dakika ya 43.

Kikosi cha Yanga kilichoanza leo Moroni na kuwachapa wenyeji 5-1

Winga machachari, Simon Happygod Msuva akaifungia Yanga bao la pili dakika ya 45 na Yanga ikaenda kupumzika inaongoza kwa mabao 2-0.

Mzambia mwingine, Obrey Chirwa akaifungia Yanga bao la tatu dakika ya 59, kabla ya Mrundi, Amissi Joselyn Tambwe kufunga la nne dakika ya 65 na Mzimbabwe Thabani Kamusoko kufunga la tabo dakika ya 73.

Ngaya walijipatia bao lao la kufutia machozi dakika ya 66 kupitia kwa Said Anfane Bourah Mohammed aliyetokea benchi kipindi cha pili.

Kikosi cha Ngaya kilikuwa; Said Mmadi, Said Hachim, Said Tothir, Adhepeau Denis Hubert, Ali Ahmada, Youssouf Ibrahim Moidjie, Zamir Mohammed, Mounir Moussa, Franck Said Abderemane, Rakoarimanana Falinurina na Chadhuili Mradabi.


Yanga SC; Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Hajji, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Justin Zullu, Simoni Msuva/Emmanuel Martin, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe/Juma Mahadhi, Obrey Chirwa na Haruna Niyonzima/Said Juma ‘Maka

Saturday, February 11, 2017

SAFU YA USHAMBULIAJI YA SIMBA SC NI MOTO WA KUOTEA MBALI


Muunganiko wa safu ya ushambuliaji ya simba sc wazidi kuimalika, baada ya matokeo ya mechi ya jana iliyochezwa uwanja wa taifa Dar es salaam kuibuka na ushindi wa magoli matatu bila kuruhusu nyavu zao kutikiswa na wapinzani wao Tanzania Prisons ya jijini Mbeya.
Muunganiko wa Laudit Mavugo na Ibrahim Ajibu wazidi kuimarika mara baada ya kupeana pasi za mwisho katika ufungaji wa magoli, ambapo Mavugo alitoa asist ya goli la pili kwa Ibrahim Ajibu kipindi cha kwanza dakika ya 28. Kipindi cha pili Ajibu naye alipiga krosi iliyozaa goli la tatu kwa simba likifungwa kwa kichwa na Mavugo na kuhitimisha idadi ya magoli matatu kwa bila.

MATOKEO YA MECHI ZILIZOCHEZWA JANA HISPANIA


 Real Betis 0:0 Valencia
 Alaves 0:6 Barcelona
Athletic Bilbao 2:1 Deportivo La
Coruna
 Osasuna 1:3 Real Madrid