Millionaire  Ads

Sunday, October 23, 2016

Tags

Simba ongezi kasi ya kufunga magoli.
Klabu ya simba ndiyo timu inayoongoza ligi kuu ya Tanzania bara huku ikifikisha alama ishirini na sita mbele ya mabingwa watetezi yanga kwa alama tano.
   Wasiwasi wangu kwa klabu ya simba ni kuridhika mapema kwa wachezaji wake pale wanapokuwa wanaongoza kwa mabao huku mchezo ukiendelea tofauti klabu yanga ambao hawachoki kufunga magoli zaidi na zaidi.
   Mechi kati yanga na kagera sugar iliyochezwa jana katika uwanja wa kaitaba wakati yanga wakiwa mbele kwa goli 4-2 waliendelea kulisakama lango la kagera kama nyuki kusaka mabao zaidi na hilo walifanikiwa kuongeza mawili zaidi na kufikia 6-2 hadi kipenga cha mwisho.
    Kwa upande wa klabu ya simba wao tatizo wakiwa wanaongoza goli moja au mbili hucheza kwa kuridhika kana kwamba wanauhakika wapinzani wao hawawezi kurudisha hayo magoli.
  Kocha au benchi la klabu ya simba wanapaswa kutambua kufunga magoli mengi kuna faida zaidi ya moja, kwanza ikitokea timu zimefungamana kwa alama magoli huwa kigezo muhimu cha nani mshindi, pili kuwa na magoli mengi kunasaidia timu kutoa mfungaji bora.
    Kwa maana hiyo nawaombeni makocha wa simba hamasisheni wachezaji kutafuta magoli zaidi kuliko kuridhika na goli moja au mbili huku dakika za mchezo zikiwa bado nyingi.
  Wito wangu timu icheze kwa tahadhari ikiepuka kutoa sare maana kufanya hivyo kutaifanya klabu ya yanga kuweza kuwatangua na pengine kuwanyang'anya tonge mdomoni.
  Klabu ya simba mnayo nafasi kubwa sana mwaka kubeba kombe na kuiwakilisha nchi katika michuano ya kimataifa ambayo hamjashiriki takribani miaka mitano.
  Rai yangu kwenu muitumie nafasi ya uwepo wa mdhamini Mohamed Dewji vizuri ili kuifanya klabu ya kimataifa zaidi kama ilivyokuwa huko nyuma ambapo ilifanya vizuri.
Mechi ya simba na toto african mlipaswa kushinda goli zaidi maana mliwazidi kila idara.
  Ombi langu kwenu, wachezaji waache kuridhika kwa goli moja au mawili maana hayo yanaweza kurudishwa na kufanya matokeo sare kitu ambacho si chema kwa timu ambayo haijatwaa ubingwa takribani miaka mitano.
Simba nguvu moja, ushindi daima

Timu ninayoipenda

Tags

Simba